8 Aprili 2015 - 19:33

Waendesha mashtaka nchini Misri wamefungua mashtaka ya mauaji dhidi ya watu 379 leo kuhusiana na vifo vya polisi na raia wakati wa kuondolewa kwa nguvu waandamanaji katika kambi ya maandamano mjini Cairo mwaka 2013.

Haijafahamika  mara  moja  ni  washitakiwa  wangapi  bado wanashikiliwa  na  polisi  lakini  ni  wimbi  la  hivi  karibuni  kabisa katika mlolongo  wa  kesi  za  halaiki  kuhusiana  na  ghasia  hizo zilizofuatia   jeshi  kuupindua  utawala  wa  rais Mohammed Mursi Julai mwaka  2013.

Waendesha  mashtaka  wanasema   washitakiwa  walishiriki  katika mgomo  wa  kulikalia  eneo  wakiwa  na  silaha  katika  uwanja  wa Nahda  mjini  humo Agosti  mwaka  2013 na  kuwashambulia  raia katika  maandamano  katika  sehemu  mbali  mbali  mjini  Cairo.

Shirika  la  kutetea  haki  za  binadamu  la  Human Rights Watch limeieleza  hali  hiyo  kuwa  ni  moja  kati  ya mauaji  makubwa  ya waandamanaji  katika  siku  moja  katika  historia  ya  hivi  karibuni.